3 Oct 2026
Ebeneza // Hata Sasa BWANA Ametusaidia // Dr Ipyana
HELP FROM ZION DAY 2 1 SAMWELI 7:4–17 Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia BWANA peke yake. Samweli akasema, “Wakusanyeni Waisraeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA.” Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga siku ile, wakasema huko, “Tumemfanyia BWANA dhambi.” Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa. Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, wakuu wa Wafilisti wakapanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti. Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, “Usiache kumlilia BWANA, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti.” Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia. Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; lakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli. Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga, hadi walipofika chini ya Beth-kari. Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Ebenezeri, akisema: “Hata sasa BWANA ametusaidia.” Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli. Nayo miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa tena kwa Israeli, tokea Ekroni mpaka Gathi; na Waisraeli wakauokoa mpaka wao mikononi mwa Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Israeli na Waamori. Naye huyo Samweli akawaamua Waisraeli siku zote za maisha yake. UNAPOFIKA MLIMANI SAYUNI, BWANA ANAKUITIKIA Unapofika Mlimani Sayuni, Bwana anakuitikia yale maombi uliyokuwa unamuomba. ZABURI 34:4–10 Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote. Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi, Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe. Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote. Malaika wa BWANA huwazungukia, Wamchao na kuwaokoa. Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia. Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Maana, wamchao hawapungukiwi kitu. Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema. “WAKATI MWINGINE ILI UWEZE KUPATA MSAADA WA KIUNGU, NI LAZIMA KWANZA UFUNGULIWE MACHO YAKO UONE VITU SAHIHI.” — Dr. Ipyana WAEFESO 1:18 Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo. “MUNGU AKIKUTANGAZIA USHINDI, USILEGEE; PANUA MIPAKA YAKO.” — Dr. Ipyana 1 SAMWELI 7:11 Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga, hadi walipofika chini ya Beth-kari. Hii inatufundisha kwamba baada ya Mungu kukupa ushindi, usiishie kwenye ushindi huo tu. Endelea kusonga mbele na kupanua mipaka yako. EBENEZER “HATA SASA BWANA AMETUSAIDIA.” Baada ya ushindi, Samweli alisimamisha jiwe na kuliita Ebenezeri, akisema: “Hata sasa BWANA ametusaidia.” Ebenezer ni ukumbusho wa msaada wa Mungu katika maisha yetu. EBENEZER KATIKA KILA ENEO LA MAISHA Kwenye biashara yako, inua madhabahu na iite Ebenezer: “Hata sasa BWANA ametusaidia.” Kwenye familia yako, inua madhabahu na iite Ebenezer: “Hata sasa BWANA ametusaidia.” Kwenye masomo yako, inua madhabahu na iite Ebenezer: “Hata sasa BWANA ametusaidia.” Kwenye kazi yako, inua madhabahu na iite Ebenezer: “Hata sasa BWANA ametusaidia.” Katika kila eneo la maisha yako, inua madhabahu na iite Ebenezer. Madhabahu yako itakuwa katikati ya adui, ikiwa ni ushuhuda kwamba Mungu amekusaidia na anaendelea kukusaidia. EBENEZER HATA SASA BWANA AMETUSAIDIA.