by United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Language

Publishing Since
2/12/2024
Email Addresses
1 available
Phone Numbers
0 available
April 29, 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunasalia hapa makao makuu.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magumu zaidi. Mzingiro huu unamaanisha kwamba familia nzima, watu saba au wanane wanalazimika kushirikiana kopo moja la maharagwe au njegere”.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limezitaka nchi za Kaskazini Magharibi mwa Afrika kuongeza ufuatiliaji na kuchukua hatua za mapema kudhibiti makundi ya nzige wa jangwani. Hii ni baada ya nzige wakubwa na makundi madogo kutoka ukanda wa Sahel kuhamia maeneo ya kusini mwa Sahara, hasa katikati ya Algeria, magharibi mwa Libya, na kusini mwa Tunisia tangu Februari hadi Machi mwaka huu.

Na katika mashinani fursa ni yake Maruping Onkemetse Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Msaada wa Familia, shirika linaloongozwa na wanawake wa asili katika Wilaya ya Gantsi, kijiji cha Chobokwane nchini Botswana anayeshiriki mkutano unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Watu wa Asili akizungumzia alichojifunza hadi sasa.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

April 28, 2025

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO. Flora Nducha na taarifa zaidi.

April 28, 2025

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.

Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi sekta ya uvuvi nchini humu inatekeleza kivitendo wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO kuhusu usalama na afya Kazini.

Na katika mashinani fursa ni yake Abdikani Haji Hassan kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambaye kupitia Mpango wa Prospects unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amejikwamua kimaisha na sasa ana ndoto ya kuenda ng'ambo ili kuendeleza ujuzi wake wa kupiga picha.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Pod Engine is not affiliated with, endorsed by, or officially connected with any of the podcasts displayed on this platform. We operate independently as a podcast discovery and analytics service.
All podcast artwork, thumbnails, and content displayed on this page are the property of their respective owners and are protected by applicable copyright laws. This includes, but is not limited to, podcast cover art, episode artwork, show descriptions, episode titles, transcripts, audio snippets, and any other content originating from the podcast creators or their licensors.
We display this content under fair use principles and/or implied license for the purpose of podcast discovery, information, and commentary. We make no claim of ownership over any podcast content, artwork, or related materials shown on this platform. All trademarks, service marks, and trade names are the property of their respective owners.
While we strive to ensure all content usage is properly authorized, if you are a rights holder and believe your content is being used inappropriately or without proper authorization, please contact us immediately at [email protected] for prompt review and appropriate action, which may include content removal or proper attribution.
By accessing and using this platform, you acknowledge and agree to respect all applicable copyright laws and intellectual property rights of content owners. Any unauthorized reproduction, distribution, or commercial use of the content displayed on this platform is strictly prohibited.