Ni muda wa kuchukua nafasi yako katika meza ya H.W nasi tutawasilisha kwako mawazo ya thamani kwa maneno ya dhahabu. Mahali pa kwanza na pekee unapohitaji kuwa kwa ajili ya ustawi wako. Karibu tujifunze vingi.
Pata nafasi ya kusikiliza mambo ya msingi sana yatakayonoa stadi zako, kukuongezea maarifa na kuchochea maendeleo yako ya kiutu. #Karibu_nyumbani.
UHURU WA KIFEDHA KUPITIA UWEKEZAJI - Emilian Busara (MBA, CPA)
Ikiwa unaanza au ni mzoefu tayari katika eneo la uwekezaji kupitia hisa, UTT, hati fungani (bonds) katika video hii mwanataaluma Mwl. Emilian Busara (MBA, CPA) katika uongozi katika biashara, miradi na fedha anakufundisha hatua kwa hatua mbinu rahisi na za kipekee za kuwekeza kwenye hisa na masoko ya fedha kwa mafanikio makubwa!
Utajifunza: jinsi ya kuchagua hisa sahihi, kuanza uwekezaji hata kama una mtaji mdogo, na siri za kukuza pesa zako polepole lakini kwa uhakika. Usikose fursa hii ya kipekee ya kujifunza hatua kwa hatua kuelekea uhuru wa kifedha kupitia uwekezaji.
Kumbuka kusubscribe ili uendelee kujulishwa pindi matoleo kama hili yanapotoka katika Youtube channel H.W TV. Fatilia kupitia H.W Podcast katika majukwaa ya sauti na kupitia mitandao yetu ya kijamii @hubofwisdom.inc au tovuti www.hubofwisdom.com/media
Anza safari yako ya mafanikio leo!
#Hisa #Utt #uwekezaji #fedha #mapato
Toleo hili limeletwa kwako na @h.w.multimedia.inc
Welcome to the home of positive vibes!
13 Nov 2024
Najma Paul - KUIJENGA NGUVU YAKO & KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
"Nianze kwa kuzungumzia hili eneo... Mitikasi ya maisha yako, kutafuta kwako, kupambana kwako. Lifestyle yako, maizingira unayoishi, vinaamua, vinahitaji na vinajenga NGUVU YAKO." Anasema Najma Paul "Fanya vitu vinavyokukwaza, vitu vinavyokukera, katikati ya hivyo vitu kuna miujiza. Niamini mimi."
Angalia toleo hili na mengine mengi kwa njia ya Youtube (H.W TV) www.youtube.com/hubofwisdom-inc
Tuma ujumbe wako wa sauti kwenda namba 0753825794 nasi tutaujumuisha katika toleo lijalo. Kumbuka unaweza kuaccess matoleo haya na kuyapakua kupitia tovuti yetu www.hubofwisdom.com/media wakati wowote pasipo bughudha ya matangazo yanayoweza kuingilia usikivu wako.
Tunathamini maoni yako, tafadhari tuandikie ujumbe wako kupitia anuani ya barua pepe info@hubofwisdom.com
#karibu_nyumbani
Welcome to the home of positive vibes!
You will love it!
26 Jan 2024
KUFIKIA KIWANGO CHA JUU ZAIDI KATIKA KILE UTAKACHOKIFANYA - Sebastian Kolowa
"Sisi sote tuna nafasi ya kustawi zaidi katika chochote tunachokifanya. Changamoto inayotukumba vijana wengi ni kwamba hatutambui na kuzifuata zile hatua muhimu zenye kutufikisha hapo. Muda ni mchache na sio sawa kwenda bila dira. Ndio maana leo nimeona niyazungumze haya yafuatayo..." Anasema Sebastian Kolowa katika mkutano wa nne wa Hub of Wisdom Community Jijini Dar Es Salaam.
Fuatilia Matoleo mengine zaidi kupitia H.W TV kwa njia ya YouTube Au sikiliza kupitia H.W PODCAST. Au tuma maoni yako kwa njia ya ujumbe wa maandishi au sauti kupitia 0753825794 ili jukwaa hili lizidi kuwa bora kwa ajili yako na wengine. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi.
Tunafurahi unapojifunza lakini tunafurahi zaidi unapofanya. Nenda duniani, kafanye zaidi na uwe zaidi!
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/hubofwisdom/message
Contact H.W PODCAST - Positive Vibes!
Guest appearances
Books guests
Based on episode analysis; this does not confirm that the show is currently accepting guests.
Host of H.W PODCAST - Positive Vibes!?
Claim your podcast to manage its listing and keep your show details accurate.
Pod Engine is an independent podcast discovery and analytics service and is not affiliated with or endorsed by this podcast. Artwork and show content belong to their owners. Full legal notice.
Explore this show Podcast research with Pod Engine