Mwanahabari mstaafu wa kimataifa, Abdu Mtullya anasema vita vya Urusi na Ukraine havistahili na huenda vikaathiri zaidi uchumi duniani, ikiwamo Afrika. Vita hivyo vimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta, Urusi ikiendelea kurusha makombora katika ngome za Ukraine, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka wa 2014.
22 Feb 2022
Mzozo wa Urusi na Ukraine; Mohamed Abdul-Rahman anachambua
Je, unafahamu chimbuko la mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, athari zake na unamaanisha nini kwa Afrika na dunia nzima? Mwanahabari/ Mhariri mstaafu na mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Mohamed Abdul-Rahman anasimulia.
20 Jan 2022
Hoja za Wahariri: Kitendawili cha mili Mto Yala - ndani ya magunia
Dunia inazidi kushangazwa na suala la mili zaidi ya 20 kupatikana ndani ya magunia katika Mto Yala. Mili hiyo ina alama na ishara za mateso. Je, waliouliwa ni akina nani na sababu za kuuliwa ni gani? Aidha, twajadili siasa za OKA vilevile usajili wa wapigakura wapya. Ali Manzu anawashirikisha wanahabari, Shisia Wasilwa na Kennedy Wandera katika kudadavua masuala haya.
14 Jan 2022
Hoja za Wahariri Podcast: Nchi bila umeme; ni njama?
Kupotea kwa umeme nchini Kenya kwa takribani siku tatu kumechochea ghadhabu. Baadhi wanahisi kwamba ni njama ya wafanyakazi fulani wa kampuni za umeme kusababisha hali hiyo maksudi. Kwamba huenda wanalalamikia mageuzi ya usimamizi katika Kenya Power, ama ni kero la wasambazaji wa kawi kulalamikia viwango vipya vya ada za umeme ambavyo ni vya chini, na kuishia wao kupata hasara. Aidha, tunajadili kujiuzulu kwa Mshirikishi wa Utawala, Bonde la Ufa, George Natembeya ili kulenga kiti cha kisiasa. Ali Manzu anawashirikisha wahariri, Charles Otieno na Kennedy Wandera katika kuyajadili masuala haya.
16 Oct 2021
Hoja za Wahariri Podcast: Ahadi za wanasiasa; watatekeleza?
Wagombea mbalimbali wa urais nchini Kenya wanazidi kutoa ahadi wanazosema watatekeleza endapo watashinda uchaguzi wa 2022. Katika podcast hii, wahariri Geoffrey Mung'ou, Roselyne Obala na mwanahabari mwandamizi, Mike Nyagwoka wanajadili iwapo ahadi zenyewe zinatekelezeka au la kwa kuweka kwenye mizani ahadi za sasa na za awali.
13 Aug 2021
Hoja za Wahariri Podcast: Raila ni chaguo la Uhuru, huku siasa zikichacha Mlima Kenya
Rais Uhuru Kenyatta amewasihi wanasiasa wa One Kenya Alliance kumuunga mkono Raila Odinga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, huku pendekezo lake likikataliwa vikali na wanasiasa hao. Aidha, wanasiasa mbalimbali wanazidi kujitokeza kwenye eneo la Mlima Kenya wakishindania udhibiti wa siasa za eneo hilo, Uhuru anapoelekea kustaafu. Je, kati ya William Ruto na Raila Odinga, ni nani atakayenufaika katika siasa za Mlima Kenya na ni nani atakayepoteza? Eneo la Mlima Kenya litaamua siasa za 2022? Wawaniaji wa urais wawateue wagombea wenza kutoka maeneo gani ya nchi? Mhariri, Geoffrey Mung'ou na wanahabari wa Standard - Chris Thairu na Mike Nyagwoka wanayapambanua masuala haya.
20 Jul 2021
HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Kivumbi kati ya Jubilee na UDA Kiambaa na Muguga
Baada ya chama kipya cha UDA kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye eneo la Kiambaa, kisha Jubilee kukishinda kiti cha uwakilishi wadi Muguga, kivumbi kinatifuka; UDA inaelekea mahakamani kutaka kura za Muguga zihesabiwe upya huku nayo Jubilee ikitaka kura za Kiambaa zihesabiwe tena. Aidha, nani ana ufuasi mkubwa Mlima Kenya baina ya Uhuru Kenyatta na William Ruto? Kuelekea 2022, farasi watakuwa wawili au watatu? Wahariri, Geoffrey Mung'ou na Odeo Sirari wanamshirikisha mwanahabari Victor Mulama aliyekuwa mashinani kuangazia chaguzi hizo, katika kujadili kwa kina masuala haya.
24 Jun 2021
HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Siasa za miungano, kulumbana na kuhamia mirengo
Je, muungano baina ya Jubilee na ODM utaafikia malengo ya kubuni serikali 2022? Aidha, kuhama au kuhamia mirengo ya kisiasa kumeshika kasi nchini bila kusahau joto la kisiasa Mlima Kenya; nani atanufaika au kupoteza kisiasa? Geoffrey Mung'ou, Odeo Sirari na Murimi Mwangi wanayazamia masuala haya.
10 Jun 2021
Hoja za Wahariri Podcast; Maraga na Mutunga wana hoja nzito - Mung'ou, Zubeida na Sirari
Uchanganuzi wa wahariri kuhusu hoja nzito za David Maraga na DkT. Willy Mutunga (majaji wakuu wastaafu) dhidi ya hulka ya Rais Kenyatta ya kukiuka sheria. Wanasema taifa linafuata mkondo mbaya na wabunge wanafaa kumtimua Uhuru mamlakani.
3 Jun 2021
HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Kura ya maamuzi itafanyika? Maendeleo ni ya kibaguzi? Mung'ou, Zubeida na Odeo wanachanganua
Wakati wa maadhimisho ya Madaraka jijini Kisumu, Rais Kenyatta aliilaumu Idara ya Mahakama kwa maamuzi aliyotaja kuchelewesha utashi wa mwananchi na kuzidisha gharama, mfano kurudia uchaguzi. Je, anakandamiza uhuru wa mahakama? Suala jingine ni iwapo kura ya maamuzi itafanyika au la kwa kuzingatia kesi za kuipinga. Na je, Uhuru anatekeleza maendeleo kwa ubaguzi? Wahariri, Geoffrey Mung'ou, Zubeida Koome na Odeo Sirari wanachambua masuala haya.
15 May 2021
Hoja za Wahariri Podcast; Mahakama Kuhusu BBI
Suala la majaji watano wa Mahakama Kuu kuharamisha mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho limechochea gumzo. Aidha, walisema kwamba Rais Kenyatta alikosea katika kuanzisha mchakato wa kuirekebisha katiba badala ya kuanzishwa na wananchi, vilevile kwamba anaweza kushtakiwa. Je, huo ulikuwa uamuzi wa kisheria au kisiasa? Wahariri wetu, Geoffrey Mung'ou, Zubeida Koome na mwanahabari nguli, Duncan Khaemba wamelizamia suala hili kwa kina.
Contact Hoja za Wahariri
Guest appearances
Books guests
Based on episode analysis; this does not confirm that the show is currently accepting guests.
Host of Hoja za Wahariri?
Claim your podcast to manage its listing and keep your show details accurate.
Pod Engine is an independent podcast discovery and analytics service and is not affiliated with or endorsed by this podcast. Artwork and show content belong to their owners. Full legal notice.
Explore this show Podcast research with Pod Engine