Je, wewe ni Mfanyabiashara, Mfanyakazi wa Taasisi ya Umma/binafsi au ni Mwanafunzi? Je, umekuwa ukihisi kuna kitu kinakosekana katika maisha yako na katika kazi unayofanya? Huenda huo ukawa wito wa mwaliko kutoka kwa Muumba wako, akikualika kujaribu mapenzi na kusudi lake katika maisha yako. Unajiuliza Sasa ufanyaje? Naam, ndiyo sababu tuko hapa. Kazi yetu ni kuhamasisha Mabadiliko ya mtu binafsi kwa kufanywa upya Akili na Mtindo wa Maisha kupitia mafundisho ya neno. Ili, uweze kuwa Wakili Mwema, Mwenye Hekima na Mwaminifu kupitia Kazi/nafasi uliyonayo kwaajili ya Ufalme wa Mungu.
Episode hii inahusu utangulizi Ili upate kufahamu InspireFikra ni nini? lengo lake ni lipi na ni kwaajili ya nani?
Nina imani baada ya kusikiliza utachukua uamuzi sahihi wa kuwa Mshirika wa kudumu wa Jukwaa hili. Utakua nami Mrs. Agnes Gabriel Sanga, Kila siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa, saa tatu kamili asubuhi. Karibu sana!
31 Jul 2020
Jifunze kutokana na makosa
Ukilichukulia kosa ulilofanya leo kama funzo unaondoa uwezekano wa kurudia tena kosa hilo hilo kesho. Lakini ni ngumu kufanya hivyo kama bado unaendelea kujihukumu kwa kutenda kosa, jisamehe, kisha jifunze.
10 Jul 2020
Je utaweza kuishi na matokeo ya uamuzi ulioufanya leo?
Historia ya maisha ya mwanadamu inaundwa na orodha ya maamuzi anayoyafanya leo. Uamuzi (choice) ni nguvu ambayo mwanadamu pekee ameruhusiwa na muumba wake kuwa nayo. Kama unavyowajibika kufanya uamuzi vivyo hivyo unawajibika moja kwa moja na matokeo ya uamuzi wako. Leo ninakuuliza swali ambalo naamini ukitafakari na ukalitumia ipasavyo, itakusaidia kufanya maamuzi sahihi zaidi katika maisha yako. Jaribu kabla hujafanya uamuzi wowote ule jiulize “Je nitaweza kuishi na matokeo ya uamuzi ninaoufanya?”.
3 Jul 2020
Je, ulipo leo ndipo ulipotaka kuwa miaka 5 iliyopita?
Binadamu ana mipango na matarajio mengi sana, lakini wakati mwingine maisha humpeleka kwenye njia tofauti mbali na ile sehem aliyokua anatarajia kufika baada ya kipindi fulani. Je ulipo sasa ndipo ulipotarajia kuwa miaka mitano iliyopita? Kama sivyo, unafanyaje? Agness anaongele hili kwenye episode ya kwanza ya Inspire Fikra. Karibu
3 Jul 2020
Thubutu kuota/Dare to Dream
Karibu. Huu ni muhtasari wa mengi mazuri na yakuhamasisha ninayotarajia kukushirikisha kupitia Podcast hii. Tunaanza na NDOTO, maana kila jambo zuri na la kushangaza unaloliona hapa duniani limesababishwa na mtu mmoja aliethubutu kuota. Ilhali pumzi bado unayo basi haujachelewa, thubutu kuota.
Contact InspireFikra
Guest appearances
Does not typically book guests
Based on episode analysis; this does not confirm that the show is currently accepting guests.
Host of InspireFikra?
Claim your podcast to manage its listing and keep your show details accurate.
Pod Engine is an independent podcast discovery and analytics service and is not affiliated with or endorsed by this podcast. Artwork and show content belong to their owners. Full legal notice.
Explore this show Podcast research with Pod Engine