Uwanja wakuzungumza mambo mbalimbali ya kuijenga jamii. Tutazungumza kwa uwazi na kwa kulenga kujenga zaidi nyanja mbalimbali za jamii kama vile; Mahusiano binafsi, urafiki, uchumba na ndoa, maadili ya jamii na fursa mbalimbali (Msingi ukiwa ni NENO la Mungu).
Tutakuwa updated na mambo mengi yanayoendelea kwenye maisha kwa ujumla huku msingi mzuri ukiwa ni NENO.
By ; Loureen Christian Production (LCP)
Linda mipaka yako, kuwa wazi mpaka wapi watu wanaweza kuingia kwenye maisha yako, ukiona mtu anavuka mstari mwambie kabisa kwamba hapa hapana! Usijiongeze kuingia sana kwenye maisha ya mtu hakuna mwanadamu anahitaji mtu wakumfuata fuata nyuma au kudhani anayajua maisha yake kuliko yeye mwenyewe.
Jali mipaka yako linda mahusiano yako. Kuhusiana vyema ni afya.
23 Mar 2023
MIPAKA KWENYE MAHUSIANO 2.
Linda mipaka yako, kuwa wazi mpaka wapi watu wanaweza kuingia kwenye maisha yako, ukiona mtu anavuka mstari mwambie kabisa kwamba hapa hapana! Usijiongeze kuingia sana kwenye maisha ya mtu hakuna mwanadamu anahitaji mtu wakumfuata fuata nyuma au kudhani anayajua maisha yake kuliko yeye mwenyewe.
Jali mipaka yako linda mahusiano yako. Kuhusiana vyema ni afya.
25 Aug 2020
KABLA HUJAANZISHA MAHUSIANO NA MTU AU KIJANA MWENZAKO, ANGALIA KWANZA MAHUSIANO YAKE NA MUNGU
Ni vizuri sana kijana wa kike au wakiume anayemuamini Kristo, kuangalia sana mahusiano ya kijana na Mungu (yani kijana anayetaka kuingia naye kwenye mahusiano ya kiurafiki au kwa lugha nyepesi ya vijana ya kimapenzi, yanayoweza kupelekea ndoa). Mara nyingi vijana hupuuzia sana hili ila yapo mambo mengi sana yanaweza yasiende sawa kama jambo hili halijaangaliwa vyema, mambo hayo tutayajadili kwenye meza kwa kiwango tutachojaliwa. Je unayetaka kutekwa naye kwenye pendo ana mahusiano gani na Mungu?? KARIBU
30 Jun 2020
VIPAUMBELE VYAKO VINAELEZA NINI KUKUHUSU!
Mtu mmoja aliwahi kusema hatma sio kitu unachokiendea bali ni kitu unachokitengeneza unahitaji kuweka vipaumbele vyako sawa(set your priorities right) vipaumbele vyako vitahakisi kwa ufasaha kabisa hatma unayoiendea.
Pod Engine is an independent podcast discovery and analytics service and is not affiliated with or endorsed by this podcast. Artwork and show content belong to their owners. Full legal notice.
Explore this show Podcast research with Pod Engine