The Chanzo Podcast is home to critical analysis and conversation around key social, political and economic issues affecting Tanzania and Africa in general. We have various guests with unique insights or experiences to share with our audience. Hosted by Khalifa Said.
Twaha Mwaipaya: Rais Samia Hawezi Kukwepa Hitaji la Katiba Mpya
Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Twaha Mwaipaya amesema kwamba kwa kazi ambayo baraza hilo imekuwa ikiifanya kwenye kuchochea uhuishwaji wa mchakato wa Katiba Mpya nchini ana imani kwamba nyaraka hiyo muhimu itapatikana kabla ya mwaka 2025.
Mwaipaya alitoa tathmini yake hiyo wakati wa mahojiano na The Chanzo yaliyofanyika katika ofisi ya chombo hicho cha habari Msasani, Dar es Salaam hapo Julai 28, 2022, ambapo alitoa maoni yake kuhusiana na masuala kadhaa ya kitaifa, ikiwemo hitaji la Katiba Mpya na mageuzi ndani ya Jeshi la Polisi.
“Kitendo cha watu waliokwamisha mchakato wa Katiba Mpya, wakafika sehemu wakazungumza kuhusu Katiba Mpya, wakati wao walisema sio kipaumbele chao, sio hatua ndogo, ni hatua kubwa,” alisema Mwaipaya wakati wa mahojiano hayo.
11 Jul 2022
Aidan Eyakuze: Ni Wajibu wa Wananchi Kusimamia Uwazi, Uwajibikaji
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema kwamba ni wajibu wa wananchi kuhakikisha kwamba Serikali yao inafanya mambo kwa uwazi ili kuchochea uwajibikaji hali inayoweza kuchangia kuboresha hali zao za maisha kiuchumi na kijamii.
Eyakuze, ambaye shirika lake linafanya kazi zake nchini Tanzania, Uganda na Kenya kuchochea uwazi na uwajibikaji serikalini, alitoa kauli hiyo wakati wa mahojiano maalum na The Chanzo yaliyofanyika ofisini kwake hapo Julai 8, 2022.
“Hii Serikali inakutumikia wewe, wewe si mtumishi wa Serikali,” alisema Eyakuze, ambaye pia ni Mwenyekiti-mwenza wa Open Government Partnership, mpango wa kidunia unaopigania uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na uwajibikaji serikalini. “Wewe ndiyo mwajiri wa hiyo Serikali.”
5 May 2022
Ben Ishabakaki: Katiba Mpya Italeta Mageuzi Kwenye Mfumo wa Utoaji Haki
Machache sana yanajulikana kuhusiana na utaratibu wa maridhiano kati ya mshitakiwa na waendesha mashitaka nje ya mijumuiko ya mawakili na wanasheria tangu utaratibu huo uanzishwe kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mnamo mwaka 2019.
Huu ndiyo msingi wa hatua ya The Chanzo kumtafuta wakili maarufu nchini Tanzania ambaye ni moja kati ya mawakili ambao wameshughulika na kesi nyingi za wateja wao kukubali kuingia maridhiano na waendesha mashitaka ili waweze kupata uhuru wao.
Huyu siyo mwengine bali ni wakili Benedict Ishabakaki ambaye katika mahojiano maalumu yafuatayo na The Chanzo anashindwa kujizuia kuelezea mchango wa utaratibu huo katika mchakato mzima wa uboreshaji wa haki jinai nchini Tanzania.
Ben, hata hivyo, ana mawazo kadhaa ambayo anadhani kama mamlaka husika zitayafanyia kazi si
Contact The Chanzo
Guest appearances
Books guests
Based on episode analysis; this does not confirm that the show is currently accepting guests.
Host of The Chanzo?
Claim your podcast to manage its listing and keep your show details accurate.
Pod Engine is an independent podcast discovery and analytics service and is not affiliated with or endorsed by this podcast. Artwork and show content belong to their owners. Full legal notice.
Explore this show Podcast research with Pod Engine