Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Waziri wa masuala ya Katiba nchini Uganda Norbert Mao, ametangaza kuwepo kwa mazungumzo ili kupata ufumbuzi wa kuendelea kuzuiwa kwa mwanasiasa mkongwe wa upinzani Kizza Besigye, anayekabiliwa na mashtaka ya uhaini. Hata hivyo, chama cha siasa cha Besigye cha People’s Front for Freedom (PFF), kinasema mwanasiasa huyo hana taarifa zozote za kuwepo kwa mazungumzo hayo. Tunachambua
21 Oct 2026
DRC: Kabila aungana na M23 kuunda vuguvugu jipya la kisiasa na kijeshi
Baada ya kuongoza nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa karibu miaka 20, rais wa zamani Joseph Kabila, ameungana na waasi wa M23 Mashariki mwa nchi hiyo na kuunda vuguvugu jipya la kisiasa na kijeshi linaloitwa FRN kumpinga rais Felix Tshisekedi na serikali yake. Nini athari za hatua hii ya Kabila na washirika wake kwa usalama na siasa nchini DRC ? Tunachambua.
14 Oct 2026
Hali ya siasa nchini Kenya mwaka mmoja baada ya kifo cha Raila Odinga
Ni mwaka mmoja, tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga. Kufariki kwake dunia, tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka 2025, kumeacha pengo kubwa kwenye siasa za nchi hiyo. Chama chake cha siasa alichoasisi cha Orange Democratic movement (ODM), kikishuhudia migawanyiko. Nini hatima ya siasa za Kenya bila uwepo wa Odinga ? Mgeni wetu wiki hii ni Alenga Torosterdt.
Contact Wimbi la Siasa
Guest appearances
Books guests
Based on episode analysis; this does not confirm that the show is currently accepting guests.
Host of Wimbi la Siasa?
Claim your podcast to manage its listing and keep your show details accurate.
Pod Engine is an independent podcast discovery and analytics service and is not affiliated with or endorsed by this podcast. Artwork and show content belong to their owners. Full legal notice.
Explore this show Podcast research with Pod Engine