Podcast thumbnail for HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

Claim This Podcast

by The New Life Mission

13 episodes
Updated Daily
Accepts GuestsHas Sponsors

Podcast Overview

Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili. Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo. Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35

Language

🇸🇼

Publishing Since

1/24/2023

1 verified contact email on file for HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

Pitch yourself as a guest, propose sponsorships, or reach out directly to the host.

Recent Episodes

Episode thumbnail for 1. Wokovu wa Wenye Dhambi Unafunuliwa Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)

January 24, 2023

1. Wokovu wa Wenye Dhambi Unafunuliwa Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)

Wigo wa mstahili wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa moja ulikuwa ni urefu unaoanzia katika kiwiko cha mtu hadi katika ncha ya kidole, takribani sawa na sentimita 45 kwa vipimo vya kisasa. Kwa hiyo, wigo wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni dhiraa 100 maana yake ni kwamba ulikuwa na urefu wa mita 45, na kule kusema kwamba urefu wake ulikuwa ni dhiraa 50 maana yake ni kuwa upana wake ulikuwa takribani mita 22.5. Kwa hiyo, hivi vilikuwa ndivyo vipimo vya Nyumba ambayo Mungu aliishi kati ya watu wa Israeli katika kipindi cha Agano la Kale. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35

Episode thumbnail for 2. Nguzo za Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)

January 24, 2023

2. Nguzo za Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)

Kifungu hiki kinaelezea juu ya nguzo, lango la pazia, mapazia ya kitani safi ya kusokotwa, mikanda, vishikizio, vikuku vya shaba, na vigingi vya shaba vya ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni mahali ambapo Mungu alikaa. Kipimo cha huo ua wa mstatili ulikuwa ni takribani mita 45 (kwa upande wake wa kaskazini na kusini) kwa mita 22.5 (katika upande wake wa mashariki na magharibi). Kimsingi, Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na umbo dogo lililokuwa na paa la lililokunjwa mara nne. Kwa upande mwingine, ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni mpana kama uwanja wa wazi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35

Episode thumbnail for 3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)

January 24, 2023

3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)

Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kisha kuzipitisha dhambi zake juu ya mnyama huyo wa sadaka kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mwanasadaka huyo, na kisha kuikinga damu yake, na kisha kuikabidhi damu hii kwa kuhani. Kuhani aliye katika zamu yake aliiweka damu hii ya mwanasadaka katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, aliyaweka mafuta na nyama ya mwanasadaka huyo juu ya madhabahu, kisha akavichoma vitu hivyo kama manukato mazuri kwa Bwana Mungu. Hata Kuhani Mkuu, ili aweze kupokea ondoleo la dhambi zake, basi alipaswa kuiweka mikono yake juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kuzipitisha dhambi zake kwa mnyama huyo mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Hii ilikuwa ni sadaka ya upatanisho iliyokuwa ikitolewa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo ilitengenezwa kutokana na mti wa mshita na kisha kufunikwa kwa shaba, na sadaka hii ya ondoleo la dhambi ilitolewa baada ya tendo la kuiweka mikono juu ya mwanasadaka na kisha kuimwaga damu huyo mwanasadaka.   https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35

13 total episodes available

Deep-dive analytics for HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

Frequently asked questions

Have a different question and can't find the answer you're looking for? Reach out to our support team by sending us an email and we'll get back to you as soon as we can.

What is HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho?

Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili. Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo. Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35

How often does this podcast release new episodes?

This podcast updates daily.

Where can I listen to this podcast?

This podcast is available on 4 platforms including Apple Podcasts, Spotify, and more. You can also use the RSS feed directly.

Does this podcast accept guests?

No, this podcast does not typically feature guests.

Legal Disclaimer

Pod Engine is not affiliated with, endorsed by, or officially connected with any of the podcasts displayed on this platform. We operate independently as a podcast discovery and analytics service.

All podcast artwork, thumbnails, and content displayed on this page are the property of their respective owners and are protected by applicable copyright laws. This includes, but is not limited to, podcast cover art, episode artwork, show descriptions, episode titles, transcripts, audio snippets, and any other content originating from the podcast creators or their licensors.

We display this content under fair use principles and/or implied license for the purpose of podcast discovery, information, and commentary. We make no claim of ownership over any podcast content, artwork, or related materials shown on this platform. All trademarks, service marks, and trade names are the property of their respective owners.

While we strive to ensure all content usage is properly authorized, if you are a rights holder and believe your content is being used inappropriately or without proper authorization, please contact us immediately at hey@podengine.ai for prompt review and appropriate action, which may include content removal or proper attribution.

By accessing and using this platform, you acknowledge and agree to respect all applicable copyright laws and intellectual property rights of content owners. Any unauthorized reproduction, distribution, or commercial use of the content displayed on this platform is strictly prohibited.